Pambano la ngumi baina ya Francis Miyeyusho na John Massamba, kutoka Malawi, lililokuwa lifanyike siku ya ijumaa, limeahirishwa.
Akizungumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, mratibu wa pambano hilo, alisema kuwa Miyeyusho, atacheza na Bondia mwingine atakayepatikana na kukubaliana na kuongeza kuwa itatangazwa siku maalum ya pambano hilo na wapi pindi taratibu zote zitakapokamilika.
Aidha Mratibu huyo, alisema kuwa Pambano hilo, limeahirishwa kutokana na bondia huyo, John Masamba, kutoka Malawi, kuonekana kutokuwa na hadhi na uwezo wa kucheza na Miyeyusho, baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na hasa katika suala zima la Afya.
Mmalawi huyo mwenye rekodi ya mapambano ya kupigwa mawili na kushinda
mawili,amecheza mwaka 1969, inaonekana ni mbovu na rekodi yake ya
utata ukilinganisha na miyeyusho mwenye mapambano 42 ya kueleweka.
kutokana na utata huo wa bondia huyo wa Malawi na kutokamilisha malipo na
vibali vyote kutoka Utamaduni na michezo.
Hivyo kwa kutambua hilo imebidi kuahirishwa kwa pambano hilo hadi hapo taratibu zitakapokamilika za upande wa vibali na kumleta bondia mzuri zaidi wa kucheza na Francis
Miyeyusho.
Mapambno mengine yatakuwepo kama kawaida katika ukumbi wa
Dar live, kati ya francis cheka na Japhet Kaseba.
No comments:
Post a Comment