Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ALhaj Dkt.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa Madrasat Nurullah Kitope Zanzibar, iliyopo Wilaya ya Kaskazini B-Unguja, Mkoa wa Kaskazini,(kulia) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,pia Mwakilishi wa jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi. Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Abdallwa Khamas na Mohamed Saidi, chini usimamizi wa mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mohamed Raza. Picha na Ramadhan Othman Ikulu.
Baadhi ya wanafunzi wa Kike wa Madrasat Nurullah ya Kitope wakiwa katika sherehe ya ufunguzi wa madrasa yao iliyojengwa kwa kiwangi kizuri ambacho kitawafanya kuwa na ari zaidi ya kusoma kwa
bidii, iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein, leo.
Baadhi ya wanafunzi wa Kiume wa Madrasat Nurullah ya Kitope wakiwa katika sherehe ya ufunguzi wa madrasa yao iliyojengwa kwa kiwangi kizuri ambacho kitawafanya kuwa na ari zaidi ya kusoma kwa
bidii, iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein, leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dkt. Ali Mohamed Shein, (wapili kushoto) akipokea risala ya wananchi na wanamadrasat Nurullah ya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja, kutoka kwa Mwalimu Juma Mohamed, baada ya kuifungua Madrasa hiyo leo mchana.
No comments:
Post a Comment