Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Samsung Tanzania jana imegawa simu 200 bure aina ya Galaxy Pocket kwa wateja wa kwanza kununua simu hizo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kuanza kuuzwa simu hizo na kutolewa bure, Meneja Mauzo na Usambazaji Kitengo cha Samsung Mobile Sylvester Manyara alisema promosheni hiyo iliyoendeshwa nchi nzima ilitangazwa kupitia redio na mitandao mbalimbali ya kijamii.
Alisema kupitia facebook waliwataka wateja wajitokeze kununu simu hizo katika maduka ya Samsung ili wapate moja bure, kwasababu ni promosheni ya siku moja.
“Hii promosheni ilikuwa ni kwa ajili ya wateja 200 tu … kwa maana tumetoa simu 400; yaani 200 za bure na 200 za kununua,”alisema Manyara huku akiwashauri Watanzania wanunue bidhaa mbalimbali za Samsung.
Naye Frank Wada mkazi wa Dar es Salaam, aliyenufaika na promosheni hiyo alisema amefarijika kununua simu hiyo na kupata nyingine bure.
“Unajua kila duka lilikuwa linapokea wateja 20; nilikwenda duka la kwanza nikakuta kumejaa nikaambiwa waliokuwepo wanatosha ndio nikaja hapa na kupata bahati hii,”alisema Wada huku akicheka.
No comments:
Post a Comment