Mshambuliaji wa timu ya Azam Fc, Kipre Tchetche (wa pili kulia) akiwachanganya mabeki wa Simba wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame hatua ya robo fainali uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Azam imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Simba, ambapo mabao yote yamewekwa kimiani na John Boko.
Kwa matokeo hayo sasa Simba itakuwa imeondolewa katika mashindano hayo, ambapo Azam sasa itacheza na timu ya AS Vita siku ya Alhamis katika hatua ya Nusu Fainali ya michuano hiyo na Yanga itakutana tena kwa mara ya pili ya APR ya Rwanda katika hatua hiyo ya Nusu Fainali baada ya timu hizo kukutana katika hatua ya robo fainali na APR ikikubali kichapo cha mabao 2-0.
Sasa je APR itakubali kipigo cha mara ya pili?
Mchezaji wa Timu ya Azam Fc, Khamis Mcha (22) akipichuana kuwania mpira na Shomari Kapombe wa Simba, wakati wa mchezo Kombe la Kagame uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Simba, Uhuru Suleiman (kulia) akichuana na beki wa Azam, Said Moradi wakati wa mchezo huo leo.
Sehemu ya mashabiki wa Azam wakishangilia timu yao baada ya kuandika bao la tatu katik mchezo huo.
No comments:
Post a Comment