Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, wakisalimiana wakati wa hafla iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake wa makampuni jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (wa pili kushoto) katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake wa makampuni jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Kennedy Bungani na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa makampuni wa NBC, Minnie Adolf Kibuta. Bwana Bungani awali alifanya mazungumzo na wafanyakazi wa NBC nchini ili kufahamiana nao.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Kennedy Bungani (wa tatu kushoto) akipiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania baada ya kufanya nao mazungumzo na baadhi ya wateja wa makampuni wa NBC jijini Dar es Salaam jana usiku.
Mshauri wa Mahusiano wa NBC, Eddie Mhina (kulia), Meneja Chapa na Matangazo, Aden Kitomari (kushoto), pamoja na mfanyakazi mwingine wa benki hiyo wakiwa katika hafla waliyoandaa kwa wateja wao wa makampuni jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Kennedy Bungani (kushoto) akipiga picha na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula Mfugale (katikati) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Godfrey Ndalahwa baada ya kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa benki hiyo na baadhi ya wateja wa makampuni wa NBC jijini Dar es Salaam jana usiku.
No comments:
Post a Comment