Pambano la ngumi la Wasanii wa Filam nchini, Jaqueline Wolper na Wema Sepetu, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana lilikuwa ni Full Commedy, baada ya wasanii hao kujiandaa na pambano hilo kwa muda ili kuonyesha ujuzi wa masumbwi ulingoni mbele ya mashabiki lukuki.
Tofauti na ilivyozoeleka kwa mchezo huu wa masumbwi hata kama wachezaji ni kina dada, basi muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani utawakuta wakijifua kujiweka sawa na kupasha misuli moto, lakini ilikuwa ni tofauti kwa mabondia hawa ambao wao badala ya kushtua misuli kupasha moto, ndo kwanza walikuwa boze kujiremba ikiwa ndiyo ndo sehemu ya kujiweka sawa kabla ya kupanda jukwaani.
Hapa ni Bondia Wolper, akijiremba kwa kujimakeup huku kucha zake zikiwa kama zinavyoonekana, yaani pambano hilo lilikuwa ni full comedy mwanzo mwisho.
Bondia wa upande wapili naye pia alikwishamaliza kujiremba hapa sasa akipozi na mwalimu wake Rashid Matumla, huku akiwa amevalia miwani yake kuuuuuuubwa.
Mafoto, aliamua kupozi kwa Snap na mabondia hao kabla ya kupanda ulingoni ili kuja kutofautisha baada ya kushuka ulingoni watakuwa katika hali gani, lakini huwezi kuamini walivyopanda ulingoni ndivyo walivyoshuka wakiwa hawana hata jasho wala kupigana hata ngumi moja.
Hapa, Mafoto, akipozi na wema, kabla ya kupanda ulingoni, hivi ndivyo alivyopanda ulingoni na ndivyo alivyoshuka.
Wolper, akikimbia kuingia uwanjani ili kupanda Ulingoni kumsubiri mpinzani wake, Wema 'Mikwara miiiiiiingi, huku akishangiliwa na umati wa watu.
Wema, naye akiingia uwanjani huku akifunika kwa kushangiliwa na umati wa watu.
Pambano lilianza kama hivi, ambapo muda wote wa raundi 2 zilizoandaliwa walikuwa ni kutishana tu, huku Wema akitoa mpya zaidi kugeuka na kutimua mbio kumkimbilia mwamuzi na kumkumbatia ili kujinusulu na kipondo.
Wema alifanya hivyo kila alipomwona Wolper, akiwa amekunja uso na kuwa siliasi huku akimtazama usoni, jambo ambalo lilimfanya Wema kuona kuwa sasa imefika kiama chake na kumrukia mwamuzi na kumkumbatia kama picha hii inavyoonekana , huku Wolper akiendelea kumuwinda.
Baada ya Wema kuona akiendelea kuwindwa na Wolper, japo amejikinga kwa mwamuzi, aliamua kuendelea kumkumbatia na kuinama na kufumba macho kabisa ili asimuone mpinzani wake, yaani alikuwa kama mtoto aliyekuwa akitishia kitu kinachomwogopesha, ambacho hajawahi kukiona.
Mwisho wa siku pambano lilimalizika kama hivi bila hata mmoja wao kupigwa hata kajingumi kamoja tu, na Mashosti hawa wakakumbatiana kwa furaha kupongezana huku wakicheka.
Tendo hili la kukumbatiana liliwachukua muda mrefu ulingoni hapo, huku mashabiki wa masumbwi wakibaki kuangua vicheko na mshangao baada ya kumalizika Comedyo hiyo ulingoni hapo.
Baada ya warembo hao kushuka Ulingoni, Jibaba hili halikuweza kuvumilia liliamua kumrukia Wolper na kumkumbatia huku likimpiga mabusu, na ndipo liliporukiwa na Mabaunsa hawa na kupelekwa panapohusika.
No comments:
Post a Comment