Habari za Punde

*JE WAJUA UKWELI CHEKA KUMKACHA KASEBA? UKWELI HUU HAPA

 Bondia Japhet Kaseba, akiingia uwanjani huku akiwa ameaongozana na wapambe wake, baada ya kuitwa kupanda jukwaani tayari kwa pambano lake na Francis Cheka, pambano lililokuwa lifanyike jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Lakini pambano hilo halikuweza kufanyika baada ya Bondia Francis Cheka, kugoma kupanda ulingoni kuzichapa na Kaseba, huku akisikika kushikilia msimamo wake 'eti hawezi kupigana na bondia ambaye hana kiwango wala uwezo wa kucheza na yeye, na pia bondia ambaye ha rekodi nzuri katika michezo yake, ambapo alisema kuwa eti amecheza michezo mitatu, amedroo 1, ameshinda 1 na kupoteza 1, wakati yeye anarekodi nzuri ya kimataifa tena akiwa amemzidi hadi uzito bondia huyo. ENDELEA KUSOMA PICHA YA PILI.
 Hapa Bondia Kaseba, akiwa katika maandalizi, kabla ya kuitwa kupanda jukwaani, huku akiwa na usongo wa kukutana na Cheka ili kulipiza kisasi na kufuta kile kilichoonekana kuzidiwa wakati wa pambano lao la kwanza lililovinjika mwaka jana katika Uwanja wa Uhuru. ENDELEA KUSOMA PICHA YA TATU.
 Hapa Cheka, akishaurina jambo na mdogo wake ili kutopanda ulingoni wakati tayari amekwishaitwa kupanda Ulingoni tayari kwa pambano na Kaseba. 

Huwezi kuamini Bondi huyu, Cheka, hadi dakika ya meisho hakupanda jukwaani kimchezo, ambpo aliamua kupanda huku akiwa ametinga mavazi yake hivi hivi kama unavyomuona, huku akiomba apewe Mic ili kuweka wazi jambo lililomfanya asipande ulingoni, lakini alinyimwa Mic na kuamua kushuka na kutimka zake. 

Ukwweli wa jambo hilo kama alivyokaririwa Bondia Cheka, ni kwamba, Cheka alikwisha tangaza toka awali kuwa hatoweza kucheza na Kaseba kwa vigezo hivyo vilivyokwishatajwa picha ya juu, ambapo alikuwa ameahidiwa kupiganishwa na Bondia kutoka nchini Malawi, jambo ambalo alikubaliana nalo na baadaye akabadilishiwa ghafla na kutakiwa kucheza na Kaseba. 

Cheka alisema kuwa, baada ya kueleza hayo aliamua kurejesha fedha na kuweka msimamo wake wa kutocheza na Kaseba, lakini waandaaji hakutaka kuweka wazi ambapo waliamua kuwadakisha baadhi ya wananiliu ili kutoandika ukweli juu ya hili, ili isije bumbuluka na kuharibu utaratibu mzima wa kurejesha fedha na gharama ambazo tayari zilikwisha tumika. ENDELEA picha ya chini.
 Lakini Ukweli ulikuwa ukijulikana tangu awali na waandaaji walikuwa wakijua kila kitu, na ndiyo maana Cheka alionekana akirandaranda tu uwanjani hapo bila kuchukuliwa hatua, jambo la kushangaza ni kwamba iwapo waandaaji kweli walimsainisha mkataba na kumlipa fedha kwa ajili ya kucheza na alifika uwanjani hapo na kugoma kupanda ulingoni, ilikuwaje wasimkamate na kumchukulia hatua?? , alipouliza Cheka sababu za kusaini mkataba na hadi siku moja kabla ya pambano akaonekana akipima uzito na mpinazni wake, alidai kuwa 'eti' ''kupima uzito na kusaini mkataba si sababu ila sababu alitaka apewe Mic ili atangaze hadharani lakini alinyimwa hivyo, ukweli amebakia nao mwenyewe na baadhi ya watu wanaofahamu, na kuwaomba radhi mashabiki wake kuwa hakukusudia kufanya hivyo na wala si kumuogopa Kaseba ila ni ubabaishaji wa Waandaaji, ambao hufanywa ili kuwanufaisha wao tu'' alisema
 Cheka akiwasiliana huku akitafuta njia ya kusepa uwajani hapo.
 Mashabiki wakimzonga Cheka asitoke uwanjani hapo.
 Cheka akitoka kwa mbinde uwanjani hapo.
 Mawe, Chupa za maji na mikojo, zilianza kurushwa, akirushiwa Cheka, kama unavyoona wapambe wake wakiwa macho juu kukwepa chupa.
Wadau wa mchezo huo wakipozi kwa picha baada ya kuona hakuna kinachoendelea uwanjani hapo.
Wadau wa mchezo huo wakipozi kwa picha baada ya kuona hakuna kinachoendelea uwanjani hapo.
Wengine walikuwa hoi baada kupata taarifa za Cheka, kutopanda Ulingoni.
Millad Ayo (kushoto) akipozi kwa picha na wanadada uwanjani hapo.
Kilichofuata ilikuwa ni burudani badala ya masumbwi, Msanii huyu ni mmoja kati wa Wabongo wanaoishi Afrika ya Kusini, akishambulia jukwaa kuwaliwaza Mashabiki wa Masumbwi, uwanjani hapo, ambaye pia aliwaboa na kuanza kuzomewa wakimtaka kutoka eneo hilo.
Chid Benz, akikonga nyoyo za mashabiki hao wenye hasira.
Diamond, akiingia kujiandaa kuingia kukonga na Josee Chamilion.
Jose Chamilion, akiingia uwanjani hapo.
Wasanii wa kikundi cha sarakasi, wakitoa burudani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.