Mwakilishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki katika Umoja wa Nchi huru za Afrika, Filbart Magere (kulia) akimkabidhi kikombe Ibrahim Obuta, baada ya timu kuibuka mshindi wa wachezaji mmoja mmoja (singles) katika mashindano ya Vishale(Darts) ya Afrika Mashariki ya yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Wachezazi wa Darts upande wa wanawake wakishangilia ushindi wao baada ya kutwaa ubingwa wakati wa mashindano ya mchezo huo ya Afrika Mashariki yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
*********************
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya mchezo wa Vishale (Darts) ya wanaume kutoka nchini Kenya imetwaa ubingwa wakati wa fainali ya mashindano ya Kimataifa ya Afrika mashariki yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi laki mbili.
Wakenya walitwaa Ubingwa huo kwa kuwagalagaza watanzania katika kiwango cha juu hivyo kuwadhihilishia kuwa Tanzania wanahitaji mazoezi ya kutosha ili kufikia kiwango chao cha maechi za kimataifa ili kupata uzoefu zaidi.
Akizungumza na wachezaji wakati wa kukabidhi zawadi mgeni rasmi ambaye ni mwakilishi wa jumuia za Afrika Mashariki katika Umoja wa nchi huru za Afrika, Flilbart Magere, aliwapongeza wachezaji wa timu hiyo kutoka Kenya kwa kutwaa Ubingwa na pia wachezaji wote walioshiriki mashindano hayo.
Magere alisema kuwa mchezo huo wa vishale sasa unazidi kupata umaarufu na hasa Afrika mashariki hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anafanya kila jitihada za kuuinua mchezo huo na kuutangaza ili upate wachezaji na wapenzi wengi.
Aidha aliipongeza Tanzania kwa kuandaa mashindano hayo ya Vishale ngazi ya Kimataifa.
Magere pia aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzani(TBL) kupitia Bia yake ya Safari Lager kwa kufadhili mashindano hayo na pia aliyaomba makampuni mengeni kuiga mfano wa kampuni hiyo.
Washindi wa pili wanaume katika mashindano hayo ya Afrika Mashariki walikuwa Lugalo ya Tanzania ambao walipata pesa taslimu shilingi laki mbili wakati upande wa Wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa pia na timu ya Nyerere kutoka Tanzania, ambayo ilizawadiwa kikombe na pesa taslimu shilingi laki mbili na nafasi ya pili ni Utawala ya Kenya ambayo ilizawadiwa shilingi laki moja.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Ibrahim Obuta kutoka Kenya ambaye alizawadiwa kikombe na pesa taslimu shilingi laki mbili na wa pili ni Wambura Msira kutoka Tanzania ambaye alizawadiwa pesa taslimu shilingi laki moja,
Kwa upande wa singles wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Rosemary Wanyori, kutoka Kenya ambaye alizawadiwa kikombe na pesa taslimu shilingi laki moja na wa pili ni Amoding Dinah, kutoka Uganda ambaye alizawadiwa pesa taslimu shilingi laki moja.
No comments:
Post a Comment