Habari za Punde

*KOZI YA MAKOCHA WA GRASSROOTS KUFUNGWA KESHO

Kozi ya makocha wa mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 inafungwa kesho (Julai 15 mwaka huu) saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Makocha hao walianza kunolewa Julai 10 mwaka huu kwenye ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam na wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wakiongozwa na Gouinden Thandoo.

Washiriki wa kozi hiyo walikuwa 35 ambao ni makocha wa timu mbalimbali zilizoshiriki mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.