Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWAFARIJI WAFIWA NA WAHANGA WA AJALI YA MELI YA SKIGET ZANZIBAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Masembe Enos (32), mkazi wa jijini Mwanza aliyekuwa akisafiri na mkewe ambaye mpaka sasa hajapatikana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Hamisa Akida (45) mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza  mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Stephano Lufyagila (22), mkazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na vijana wawili, Hans Manoni (kulia) na Nsunga Joseph, waliokuwa wakisafiri na wenzao wawili ambao wamefariki katika ajali hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsalimia Salome Abeid Mwambaga (33) mkazi wa jijini Arusha, mfanyakazi wa Kampuni ya Atomic Enegy Commissioner, aliyekuwa akisafiri kuelekea Pemba kikazi ambaye pia amepoteza vifaa vya kazi na Document zake zote muhimu katika ajali hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kumpa pole kuhusu ajali ya Meli ya Skiget mali ya Kampuni ya seagull, iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe.
 Wananchi wakiwa wamepanga foleni kuelekea kutambua miili ya marehemu katika Viwanja vya Maisara leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujionea shughuli hizo katika viwanja vya Maisara mjini Unguja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumjuika na wananchi katika moja ya familia iliyopotelewa na ndugu katika ajali hiyo, mjini Zanzibar leo mchana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.