Rais wa LiberiaEllen-Johnson-Sirleaf.
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS wa Liberia, Ellen John-son Sirleaf, amewataka viongozi wa nchi za Afrika kufanya jitihada za kuhakikisha wanatenga rasilimali za kutosha za kuweza kupambana na ugonjwa wa Malaria ili ifikapo mwaka 2015 Bara la Afrika lifanikiwe kutokomeza ugonjwa huo kwa asilimia zero.
Rais Jakaya Kikwete. |
Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais huyo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Ofisi za Umoja wa Viongozi wa Afrika wa Kudhibiti Malaria(ALMA) iliyopo katika Kituo cha Mkakati wa Kupambana na Malaria(Ceemi), jijini Dares Salaam.
Alisema lengo kubwa la ALMA ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 Bara la Afrika linaondokana na ugonjwa huo ikiwemo vifo vinavyosababishwa na Malaria .
“Tunaweza kufanya hivyo ili tuweza kufanya tunatakiwa kuchukua hatua za kuwa na rasilimali za kutosha na kuzitawanya katika vituo vya afya kama ilivyo katika azimio letu la Abuja.” Alisema Rais Hellen.
Aliongeza kuwa jitihada hizo zitafanikiwa kwa kuboresha usimamizi bora wa mfumo wa fedha ili kuweza kukabiliana na tatizo la uhaba wa fedha kiasi cha dola za Marekani bilioni 3.2 .
“ Tunatakiwa kuboresha mifumo yetu ya fedha ili kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kupambana na ugonjwa wa Malaria mfano dawa na utoaji wa vyandarua bure, utafiti na kuwa wabunifu wa kutafuta njia za kukabiliana na uhaba wa fedha ili tuweze kutimiza lengo la kuwa na asilimia zero ya Malaria ifikapo mwaka 2015. ” alisisitiza.
Rais huyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALMA alisema baadhi ya nchi zimefanikiwa kutimiza lengo hilo la Abuja, ambazo ni Msumbiji, Togo na Rwanda.
Aliongeza kuwa bara hilo limefanikiwa kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo kwa asilimia 33 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita alisema.
Kwa upande wake Rais Jakaya Kikwete alisema bara hilo, linaongoza kwa vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa asilimia 89 na kuwa na wagonjwa kwa asilimia 83.
“Tukikusanya nguvu za pamoja naamini tunaweza kufanikiwa. Tumeaanza vizuri nguvu za pamoja zitatuwezesha kufatuta vifaa pamoja ili kila nchi viweze kupelekwa.
Alisema kupitia ALMA wamefanikiwa kutoa vyandarua bure milioni 400.
Wakati huo huo Rais Kikwete alisema Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano na ALMA ili kufikisha malengo ya kupambana na ugonjwa huo.
Katibu Mtendaji wa ALMA, Joe Pumaphi alisema dola za Marekani bilioni 12 hutumika kila mwaka katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Huku akihoji ni kwanini fedha hizo ziendelee kutumika.
Aidha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DK. Hussein Mwinyi alisema nchini Tanzania ugonjwa huo bado unaongoza kwa kusababisha vifo vya mama wajawazito na watoto. Hivyo kesi zinazoripotiwa ni za watu milioni 12 na vifo watu 60,000 hadi 80,000 kwa mwaka.
Alisema Tanzania imefanikiwa kutokomeza ugonjwa huo kwa asilimia 50 kwa utoaji wa vyandarua vilivyo na dawa bure kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano milioni tisa na kaya milioni 17.6.
Alisema changamoto iliyopo ni kuwa na uwezo wa kununua dawa na vyandarua kwa kutumia fedha za ndani.
Katika hatua nyingine Dk. Mwinyi alisema serikali itaendelea kusimamia uuzaji wa dawa mseto ili kuhakikisha zinapatikana kwa bei inayostahili.
No comments:
Post a Comment