Habari za Punde

*SHILINGI KUAMUA MSHINDI WA KWANZA NA WA PILI WA KUNDI B KATI YA AZAM NA MAFUNZO KESHO

 Mshambuliaji wa timu ya Azam Fc, Kipre Tchetche (kushoto) akiwatoka mabeki wa Tusker wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 0-0 na kuifanya timu ya Tusker kutolewa katika mashindano hayo baada ya kumaliza mchezo huo ikiwa na Pointi 2 huku ikiwa haina goli hata moja la kufunga, wakati Azam imemalia mchezo huo ikiwa na Pointi 2 na goli 1 sawa na Mafunzo ambao nao wana Pointi 2 na goli 1. 

Kwa matokeo hayo sasa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF, kesho litarusha shilingi mida ya saa sita mchana ili kuamua nani mshindi wa pili na wa kwanza kati ya timu ya Azam na Mafunzo, ambapo mshindi wa pili kati atakayepatikana kati ya hizo atacheza na Yanga. 

URA atachea na APR, Yanga na mshindi wa pili wa kundi B Julai 17, Atletico na mshindi wa pili wa kundi A, B1 atakayepatikana kesho kucheza na mshindi wa tatu wa kundi A.
Beki wa Azam Fc, Erasto Nyoni (kulia) akimtoka beki wa Tusker, Jockins Atudo, wakati wa mchezo huo leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.