Habari za Punde

*VIINGILIO KATIKA MECHI ZA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME


Michezo yote ya Nusu fainali za kuwania Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) mwaka 2012 zinachezwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Azam na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zitacheza nusu fainali ya kwanza kuanzia saa 8 kamili mchana, na kufuatiwa na nusu fainali ya pili kati ya Yanga na APR ya Rwanda itakayoanza saa 10 kamili jioni.

WAKATI HUO HUO TFF KUFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KESHO.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho litakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika ofisi za TFF saa 5 kamili asubuhi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.