Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amefiwa na shemeji, ambapo amekabidhi kiti cheke ndani ya Bunge kwa Samuel Sitta hii leo, ili kuondoka kwenda kushiriki shughuli hiyo ya msiba.
Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Jenista Mhagama alitoa taarifa hiyo bungeni mchana huu wakati akiahirisha kikao cha asubuhi cha mkutano uliokuwa ukijadili hoja ya bajeti ya Wizara ya Maji.
Mhe. Jenista alisema kuwa Pinda hatokuwepo bungeni kwa vile amekwenda kushughulikia msiba huo.
Kutokana na msiba huo, Waziri Mkuu amemteua Waziri wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta, kuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni kuanzia leo Julai 10, hadi Julai 15 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment