Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur-an yaliyoshirikisha nchi 13, ambapo mshindi alikuwa ni Abdulrahman Salis Ahmad (18) kutoka Nigeria, aliyeshinda kwa jumla ya Pointi 96.12 na kunyakua kitita cha Dola za Kimarekani, 3150.
Mmoja kati ya washiriki wanne walioiwakilisha Tanzania, katika fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur-an, yaliyoshirikisha nchi 13, Nassor Muhammad, akisoma Qur-an wakati akishiriki katika fainali za mashindano hayo ya Kimataifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo.
Mshiriki kutoka Jumuiya za Umoja wa Falme za Kiarabu, U.A.E Ahmad Wajih, akisoma Qur-an, wakati wa fainali hizo.
Mshiriki kutoka Egypt, Mohammad Saad, akisoma Qur-an, wakati wa fainali hizo.
Mshiriki mdogo kuliko wote katika fainali hizo kutoka China, Suleyman Ahmad (9), akisoma Qur-an, wakati wa fainali hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Dola za Kimarekani 1250, mshindi wa tatu katika fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, Ijaaz Mukaddam (22), kutoka Afrika ya Kusini, aliyepata jumla ya Pointi 95.08.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi funguo ya Pikipiki, mshindi wa kwanza kwa watanzania, Mohammed Omar Mkilalu, baada ya kutangazwa washindi wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mshiriki mdogo kuliko wote katika mashindano hayo ya Qur-an, ya kimataifa, Suleyman Ahmad (9) kutoka China, aliyeshiriki katika fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti Ustaadh Muhammad Abdullah Balarabe, aliyeongozana na mshiriki mshindi wa kwanza katika fainali za mashindano hayo ya Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi za Dini ya Kiislamu na washindi wa tatu Bora wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa Mufti wa Tanzania, Sheikh Ally Muhidin Mkoyogole, baada ya kumalizika kwa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an ya kimataifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, wakiondoka katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
No comments:
Post a Comment