Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MABANDA YA MAONYESHO YA NANE NANE MJINI DODOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal, Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakiangalia Mhogo aina ya Mumba wenye umri wa miaka (3) wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana.Wa pili (kulia) ni Mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mbegu ya mizabibu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi mashine za kukamulia miwa zinavyofanya kazi, kutoka kwa Mjasiliamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, maonyesho ya Nane Nane kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana.Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo jinsi ya uzalishaji wa zao la Zabibu kutoka kwa Ofisa Mtafiti Msaidizi wa Kilimo wa Kanda ya Kati Dodoma, Richard Malle, (wa pili kulia).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.