Wayne Rooney akiugulia jeraha alilopata juu ya goti la kulia alipoumizwa na mchezaji, Hugo Rodallega wa Fulham, siku ya Jumamosi iliyopita.
Rooney, sasa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili akijiuguza jeraha hilo, badala ya mwezi mmoja uliokuwa umetangazwa awali.
Mshambuliaji huyo tegemezi kwa timu ya Manchester Utd na timu ya Taifa ya England, anaweza kukosa jumla ya mechi 14 za klabu yake na timu yake ya taifa inayojiandaa kuanza kampeni ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2014 mwezi ujao.
Aidha Rooney, hatakuwepo katika kikosi kitakachoikabili Liverpool, Septemba 23, na mechi mbili za timu yake ya Taifa ya England za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2014, dhidi ya Moldova na Ukraine pamoja na mechi za kwanza za makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment