KLABU ya Dar Young Africans ya jijini Dar es Salaam, leo imewasilisha jumla ya majina ya 28, ya wachezaji kwa shirikisho la soka nchini TFF, kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara, nchini inayotarajia kuanza mapema septemba mosi.
Katibu mkuu wa timu ya Yanga, Mwesigwa Selestine, amesema kuwa tayari leo wamewasilisha majina ya wachezaji wote 28 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu, baada ya benchi la ufundi la timu hiyo kuridhia kuwatumia wachezaji wote.
Aidha katika usajili huo uliowasilishwa leo, umeambatana na usajili wa wachezaji wa timu ya vijana U-20 ambao ni wachezaji mahiri wa timu ya Taifa Saimon Msuva na Frank Domayo.
Maji ya Usajili kamili kwa timu ya wakubwa ni kama ifuatavyo:
Walinda Mlango: Yaw Berko, Ally Mustafa 'Barthez' na Said Mohamed.
Walinzi wa pembeni: Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika.
Walinzi wa kati: Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Mbuyu Twite, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo.
Viungo wa ulinzi: Athuman Idd 'Chuji', Juma Seif Kijiko na Salum Telela.
Viungo wa pembeni: Nizar Khalfani, Shamte Ally, Idrisa Rashid na Omega Seme.
Viungo washambuliaji: Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari.
Washambuliaji: Said Bhanaunzi, Hamis Kiiza 'Diego', Didier Kavambagu na Jeryson Tegete.
Majina hayo yanakamilisha jumla ya wachezaji 28 kwa timu ya wakubwa.
Kikosi cha U-20 kina jumla ya majina 22 ambao ni:
Walinda Mlango: Geofrey Nyalusi na Yusuf Abdul.
Walinzi: Said Manduta, Zuberi Juma, Said Mashaka, Benson Michael, Issa Ngao, Rashid Said.
Viungo: Frank Domayo, Omary Nasry, Clever Charles, Mwinyi Bakari, Mpenda Abdallah.
Washambuliaji wa pembeni: Abdulahman Ally, Hussein Moshi, Abdallah Salum, Rehani Kibingu.
Washambuliaji: Saimon Msuva, George Banda, Notikely Masasi, Suleiman Ussi, Kassim Jongo.
NB: Frank Domayo & Saimon Msuva usajili wao umepelekwa katika usajili wa U-20 lakini wataitumikia timu ya wakubwa.
No comments:
Post a Comment