Askari wa Kampuni ya Ulinzi anayelinda katika Jengo moja ya benki iliyopo Barabara ya Bibi Titi eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam, alienda chini na Kibaka aliyekuwa akimuokoa kutoka mikononi mwa wananchi wenye hasira kali, baada wananchi hao kuanza kumpa kichapo cha haja baada ya kibaka huyu kukwapua Ipad katika moja ya gari lililokuwa katika foleni lililokuwa likiendeshwa na Mwanamama wa Kihindi na kudakwa na mmoja wa dereva aliyekuwa nyuma ya gari hilo wakati akijaribu kukimbia na kumuitia mwizi. Baada ya sauti hiyo ya kuitiwa mwizi wananchi waliitikiwa wito na kuanza kumuandamisha ambapo hakufanikiwa kufika mbali walimdaka na kuanza kumpa kichapo hadi alipoingilia kali askari huyo na kumuokoa kisha kumfungia ndani ya geti alilokuwa akilinda.
Kichapo kinaendelea......
Askari huyo akijitahidi kumuwahisha kumuingiza ndani ya geti....
Akifunga geti baada ya kufanikiwa kumuokoa kutoka katika msiti wa wananchi wenye hasira kali, huku wananchi hao wakipiga kelele kuwa waachiwe wammalize...
No comments:
Post a Comment