Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kumpongeza Mwakilishi mpya wa Jimbo la Bububu Mhe. Hussein Ibrahim Makungu,(kulia) CCM,kwa kushinda uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,kushiriki katika kikao cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar,kilichofanyika leo. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume,akisalimiana na kumpongeza Mwakilishi mpya wa Jimbo la Bububu Mh,Hussein Ibrahim Makungu,(kulia) CCM,kwa kushinda uchaguzi mdogo wa jimbo hilo,alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,kushiriki katika kikao cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar,kilichofanyika leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,kwa pamoja wakiwa wamesimama kabla ya kuanza kikao cha siku moja cha Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar,kilichofanyika leo katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,wakiwa katika kikao cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume,wakiwa katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,kilipofanyika kikao hicho leo.
No comments:
Post a Comment