Habari za Punde

* UBALOZI WA MAREKANI NCHINI LIBYA WATEKETEZWA

cairo protestsAfisa mmoja wa ubalozi wa Marekani ameuawa na wengine wamejeruhiwa wakati kundi la watu waliojihami na silaha walipovamia jengo hilo mjini Benghazi.

Maandamano pia yamefanyika mjini Cairo, Misri Inaaminika kuwa watu hao walikuwa wanaandamana kulaani filamu mmoja iliotengenezwa nchini Marekani ambayo wanasema inamkejeli Mtume Mohammed.
Jengo hilo liliteketezwa kabisa na wandamanaji hao waliokuwa na hasira.

Maandamano hayo yalichochea makabiliano kati ya vikosi vya serikali na kundi la wanamgambo maarufu kama Ansar al Sharia brigade, mjini Benghazi.

Msemaji wa serikali ya Marekani, amelaani kitendo hicho na ameongeza kuwa wanashirikiana na idara ya usalama nchini Libya kuimarisha usalama kwenye balozi zake.

Taarifa zinasema kuwa wakaazi wa mji mkuu Tripoli, wamekuwa wakishawishiwa kupitia ujumbe kwenye tovuti za kijamii wafanye maandamano lakini hakuna aliyejitokeza.

Sehemu ya filamu hiyo inasambazwa kupitia mtandao wa Youtube kwa lugha ya kiarabu.

Maandamano sawa na hayo pia yamefanyika mjini Cairo nchini Misri. Kundi lingine la watu limeingia kwenye ubalozi wa Marekani na kuteketeza bendera ya nchi hiyo.

Taarifa kutoka Cairo zinasema, maelfu ya Waislamu na Wakristo wameungana kulaani filamu hiyo. Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa kwenye maandamano hayo yaliofanyika Misri. Habari kwa hisani ya BBC Swahili.com

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.