BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' yupo katika mazoezi mazito kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Jonas Segu utakalofanyika October 14 siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese.
''Tunamuhandaa vizuri ili aje kuwa bondia bora wa masumbwi hapa nchini kwani kama unavyojua, kuna staili nyingi za mazoezi ambazo anapewa ili kumkabili mpinzani wake kwa kuwa tunamjua vilivyo'' alisena Super D
Super D aliongeza kuwa mazoezi anayofanyishwa 'King Class Mawe' kwa sasa hakuna bondia anayeweza kumfikia kwa kuwa hivi sasa tayari ameshavuka viwango na anacheza katika uzito wa Kg 60 amekuwa tishio kwa mabondia wezake baada ya mchezo wake wa mwisho kumdunda SakoMwaisege kwa K,O raundi ya tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar-Es-Salaam.
No comments:
Post a Comment