Habari za Punde

*MKUTANO WA MAKTABA KWA MAENDELEO WAFUNGULIWA LEO DAR

Mratibu wa  Mradi wa chama cha wakutubi kutoka Finland (TLF) Marjatta Lahthi akitoa taarifa yake katika ufunguzi wa mkutano wa  maktaba kwa maendeleo  jijini Dr es Salaam leo ambapo umewashirikisha zaidi ya watu 80  wakiwemo wadau wa maktaba pamoja na wajasiriamali kutoka Tanzania, Kenya,Finland,Gemany, Italy na United Kingdom.  Mradi huo kupitia maktaba pamoja na mtumizi ya teknolojia ya ICT utawawezesha kupata habari mbalimbali za shughuli zao za kila siku.
Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Alli Mcharazo akitoa taarifa yake  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Maktaba kwa maendeleo leo jijini Dar  es Salaam ambao umefunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na  Mafunzo ya Ufundi Selestine Gisimba (hayupo pichani).
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Libraries for Development wakiwa katika mkutano huo wa siku mbili uliofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na  Mafunzo ya Ufundi nchini Selestine Gisimba (hayupo pichani ) leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umewashirikisha washiriki wapatao 80 kutoka nchi ya Tanzania, Kenya, Finland,  Germany, Italy na United Kingdom. Mradi huo wa Maktaba kupitia teknolojia ya  ICT utawawezesha kuwasaidia  kupata elimu na taarifa mbalimbali za shughuli zao za kila siku.

 Washiriki wakikagua vitabu.
Picha ya pamoja. Picha zote na Mwanakombo Jmaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.