Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi, Patrick Mfugale (kushoto) na Mtendaji Mkuu kutoka kampuni ya ujenzi ya China Railway 15 Bureau group Corporation (CR15G) Zhang Tonggang, wakitiliana saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kilombero lenye urefu wa mita 384 na ujenzi wa barabara zake za miingilio za lami ( kilometa 9.142), ambapo ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 53.2 . Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Dkt, John Magufuli (mwenye miwani) na kulia kwake na katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Herbert Mrango.Pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Tanroads , Bibi Hawa Mmanga,Mbunge wa Mikumi- Abdul Salim Ameir na Mbunge kutoka Morogoro Kusini Innocent Kalgeris. )
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kulshoto) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G) Bw, Zhang Tonggang (kulia) wakibadilishana hati baada ya kuweka saini kwaajili ya ujenzi wa darala la Kilombero mkoani Morogoro, Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment