Habari za Punde

*ZOEZI LA KUKAMATA MAGARI YA SERIKALI YANAYOTUMIA NAMBA BINAFSI KUFANYIKA NCHI NZIMA KARIBUNI

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo  kusisitiza  utaratibu wa usajili wa magari ya Umma kuwa, unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote.Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba  za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .  Baada ya hapo Operesheni hiyo itaanza kukamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma,Vileve kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma (kulia) ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani katika jeshi la Polisi  nchini Kamanda James Mpinga.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.