Wanajumuiya!
Tunamshukuru M/Mungu kwa kuweza kuhimili dhoruba ya "Super storm Sandy". Pole sana kwa waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki. Tunawashukuru sana Wanajumuiya kwa ushirikiano waliotoa kwa wanajumuiya waliohitaji msaada, kwa kutoa malazi na chakula na ukarimu mkubwa ambao hujawahi kutokea. Tuendelee na moyo huu. Tunafahamu itachukua muda kurudi katika hali ya kawaida, tafadhali wasiliana na jumuiya kama utahitaji msaada au ushauri wowote. Tupo pamoja na wewe.
Bakia salama.
Shabani Mseba
The Secretary i.e
No comments:
Post a Comment