Wimbo wa "Mama Kimwaga" wa Ngoma Africa band
Wazua baraha ! Jimama Pesa lamsaka Kamanda Ras Makunja wa FFU ! kwa bakora mitaani !
Bremen,Ujerumani.
Katika hali ya utatanishi kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja wa FFU amejikuta akipewa mashaka ya maisha na mwanamama moja kisa wimbo "Mama Kimwaga" ! ambao takribani mwezi mzima wimbo huo na nyingine za bendi zimekuwa zikipigwa mara kwa mara na kituo cha Radio Funk haus inayorusha matangazo mjini Bremen,Ujerumani.
Mwanamama huyo ambaye aliguswa sana na ujumbe wa wimbo huo, aliamua kutinga katika ukumbi wa mazoezi wa bendi hiyo mjini Oldenburg,mkononi akiwa na bakora ! mdomoni yakiwa yanamtoka maneno ya hasira.
Alisikika Mama huyo akidai kuonana na mkuu wa kikosi kazi cha Ngoma Africa aka FFU kamanda Ras Makunja,kwa bahati mbaya alijibiwa na wanamuziki waliokuwa eneo hilo, kuwa Kamanda hayupo.
Baada ya kupata jibu hilo, Mama huyo na kuulizwa kulikoni? Jimama Pesa huyo alisikika akidai kuwa alikuja kumtia adabu Kamanda Ras makunja wa FFU.
Jimama pesa huyo aliendelea kukoroma na kutema kibesi kuwa wimbo ule wa "Mama Kimwaga" ujumbe wake unamnyima raha jimama huyo mwenye kuongea kiswahili fasaha kinachoonyesha kuwa anatoka nchi jirani kwa watani wa jadi wa Tanzania.
Aidha Jimama pesa huyo, amedai kuwa akutegemea kabisa kama wimbo ule wa "Mama Kimwaga" ungepelekwa tena kwa maDJ wa redio Bremen na kurushwa hewani Ujerumani kote kwa kupitia sauti ya Funk Haus Europa, wanamuziki aka "maafande" wa Ngoma Africa band wakimtetea Boss yao Kamanda Ras Makunja,wamedai kuwa hawezi kuingilia uhuru wa ma Dj wa redio kwa CD hiyo ilikuwapo pale redio siku nyingi,na katika CD hiyo aliyeimbwa ni "Mama Kimwaga" sasa inakuaje ? kamanda asakwe na bakora ka kushutumiwa kuwa anazuia ridhiki ya mahitaji ya starehe ya jimama pesa huyo.
Wanamuziki wa ngoma africa wanamuhoji mwanamama anayemsaka kwa bakora kamanda wao Ras Makunja,ambaye mara nyingi anadaiwa kuwa ni mtunzi na mwimbaji mwenye darubini kali. UNAWEZA KUUSIKILIZA WIMBA HUO KUPITIA www.myspace.com/thengomaafrica na www.reverbnation.com/ngomaafricaband
No comments:
Post a Comment