Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Daktari Bingwa wa (kulia) macho wa Watoto, kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, ‘Optometrist’, Judith Mwenda, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika Mabanda kujionea shughuli za upimaji macho kwa watoto, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa miaka mine wa ‘Kuona ni Kuamini’ maalum kwa ajili ya kuboresha afya ya macho kwa watoto kwa Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, uliodhaminiwa na Benki ya Standard Chartered, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Agrey Manry, (wa tatu kushoto) ni Mtoto Abubakar Siaba Kaim, mkazi wa Keko Mwanga, akipimwa macho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Paulina Mvella, wakati akimpima mtoto, Brayan Paul (7) mkazi wa Kigamboni, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika Mabanda kujionea shughuli za upimaji macho kwa watoto, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa miaka mine wa ‘Kuona ni Kuamini’ maalum kwa ajili ya kuboresha afya ya macho kwa watoto kwa Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, uliodhaminiwa na Benki ya Standard Chartered, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Agrey Manry.
Makamu, akihoji jambo.....
Uandikishwaji wa watoto wenye mahitaji ya kupimwa macho ukifanyika viwanjani hapo.
Upimaji kwa watoto, ukiendelea....
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mpango wa miaka mine wa ‘Kuona ni Kuamini’ maalum kwa ajili ya kuboresha afya ya macho kwa watoto kwa Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, uliodhaminiwa na Benki ya Standard Chartered, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
Shughuli ya upimaji ikiendelea kutolewa kwa watoto waliofika katika Viwanja hivyo vya Mnazi Mmoja.
Daktari Bingwa wa (kulia) macho wa Watoto, kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, ‘Optometrist’, Judith Mwenda, akimpima mtoto, Abubakar Siaba Kaim, mkazi wa Keko Mwanga. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo, Amina Maulid.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, wakitoa burudani kwa kuimba wimbo wao mmalum, wa kuhamasisha wazazi kuwapima watoto wao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini maalum ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mpango wa miaka minne wa ‘Kuona ni Kuamini’ maalum kwa ajili ya kuboresha afya ya macho kwa watoto kwa Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, uliodhaminiwa na Benki ya Standard Chartered, uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
No comments:
Post a Comment