Habari za Punde

*MIYAYUSHO KUZICHAPA NA NASSIB KUWANIA UBINGWA WA WBF DESEMBA 9


Picha ya juu:- Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho, wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha pambano lao la ubingwa wa WBF litakalofanyika Desemba 9, mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam.

Picha ya chini:- Mwandaaji wa pambano hilo, Mohamed Bawazir (katikati) akiwa ameshika mkanda na mabondia Nassibu Ramadhani (kushoto) na Fransic Miyayusho (wa pili kulia) wengine kulia ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa ambao na wasimamizi wa mpambano huo na Kushoto ni Mratibu Paul Kunanga na Kocha wa Nasibu Christopher Mzazi.
*******************************************
KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho, mpambano huo utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba,

Aakizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Bawazir,amesema  kuwa amewakutanisha mabondia hao kutaka kujua nani zaidi ya mwenzake kwa kuwa viwango vyao vina fanana na vinatambulika kimataifa hivyo amewataka watanzania kujitokeza kuwapa sapoti hususani kudhamini wa mchezo huo wa masumbwi.

Udhamini tunapoomba sehemu ya makampuni mbalimbali ukienda wanasema atuhusiki na mchezo huo,Wengine wanasema kabisa wadhamini wa michezo wakati wanabagua michezo mingine kama ngumi awapewi kipaumbele kabisaa

amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza siku ta 9 Desemba kuja kuangalia ngumi ili zisonge mbele watakaosindikiza mpambano huo wa masumbwi ni Fadhili Majia VS Juma Fundi Moh'd Rashid Matumla VS Doi Miyayusho Ibrahimu Class 'King Class Mawe' VS Said Mundi wa Tanga
Fred Sayuni VS Deo Samweli Hassani Kidebe VS Baina Mazola

Mapambano yote ya utangulizi ni mazuri na vijana wanaotakiwa kuendelezwa katika elimu ya masumbwi Duniani ili wawe mabondia wazuri.

Mpambano huo umedhaminiwa na JB BELMONT HOTEL gazeti la Jmbo Leo, Times FM,Na wengine wameobwa kujitokeza katika udhamini huo kwa mawasiliano zaidi:- 
 0716 332933
 0784 426542.

KWA AJILI YA KUTOA SAPOTI YA AINA YOYOTE PAMOJA NA USHAULI KATIKA MPAMBANO HUU.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.