Habari za Punde

*SELEMAN SAID KUZICHAPA NA CALED AMAEINDA KESHO


Mpambano kati ya bondia SELEMANI SAIDI VS CALED AMAEINDA wa Kenya linatalajia kuchezwa kesho  katika uwanja wa KINESI uliopo katika jimbo la Ubungo, tarehe 10 -11-2012 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao huu leo jioni Rais wa PST Emanuel Mlundwa amethibitisha kuwepo kwa mpambano huo ambapo CALED AMAEINDA wa Kenya amewasili kwa ajili ya kupambana na Seleman Toll siku hiyo.

 Taarifa zilizotolewa na moja ya chama cha masumbwi kuwa hatambui mpambano huo ndio mana PST ikachukua jukumu la kuingilia kati na kusimamia ili kufanyika kwa mpambano huo. 

Mlundwa alisema mabondia ndio wanaopigana hivyo hana sababu ya kusitisha mpambano huo usifanyike kwa baadhi ya watu wachache wasioutakia mema mchezo wa masumbwi kuleta fujo za uongozi wa hapa na pale.

''Mpambano huo utafanyika kesho kuanzia saa kumi jioni kama kawaida na kuendelea na baadhi ya wachezaji wanaocheza utangulizi wamepima uzito leo kwa ajili ya mpambano huo na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia masumbwi hayo''. alisema Mlundwa

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.