Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi fedha za mkopo kutoka mfuko wa vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe (kushoto) akimsomea taarifa fupi ya mkoa wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia ) alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yuko mkoani Kagera kwa ajili ya kuangalia jinsi fedha za mkopo kutoka mfuko wa Maendeleoa ya vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (hayupo pichani) wakati akiongea nao kuhusu umuhimu wa kuwafuatilia vijana kwa ukaribu katika Kata na kuweza kuwafundisha na kuwashirikisha katika miradi ya maendeleo
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment