Habari za Punde

*SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA CLUB BILICANAS NA MIAKA 13 YA CLOUDS FM


Bendi ya muziki ya dansi ya Sky Light ikitumbuiza katika sherehe za kutimiza miaka 20 ya Club Bilicanas na miaka 13 ya Clouds FM. 
Sherehe hizo zilipambwa na shamrashamra za aina mbalimabli ikiwemo kukati keki pamoja na kufungua shampeni
Mwakilishi wa Clouds FM, Wasiwasi Mwabulambo akizungumza katika hafla hiyo.
 Tukate keki
 Mmoja kati ya wafanyakazi wa kwanza wakati Bilicanas Club inaanzishwa miaka 20 iliyopita, Monika Victor akimlisha keki, Dk. Lilian Mtei wakati wa hafla ya kutimiza miaka 20 ya klabu hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. 
 Maandalizi ya keki
Dk. Lilian Mtei, akimlisha kipande cha keki Meneja Msaidizi wa Vinywaji wa Club Bilicanas, Amandus Agant wakati wa sherehe hiyo ya Bilicanas Club kutimiza miaka 20.
 Monica Victor akigawa keki kwa wadau waliofika katika sherehe hizo.
 Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka, akiwa na Khadija Kalili pamoja na wadau wengine. 
Watu wa mataifa mbalimbali wakicheza muziki katika ukumbi wa Bilicanas.
********************************* 
Na Andrew Chale

WADAU  mbalimbali  wa burudani  usiku  wa kuamkia jana walifurahia kwa pamoja  na kula keki ya miaka 20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka 13, ya Clouds Fm,  iliyoambatana na shamrashamra mbalimbali ndani  na nje ya  ukumbi huo.

Sherehe hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group, Dk. Lilian Mtei  ambapo aliwashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu hiyo, tangu 1992. “Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora siku zote|” alisema Mbowe.

Mtei pia aliwashukuru wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha ukumbi huo kufikia hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa wafanyakazi  waliokuwapo  tokea inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na hatimaye  kukata keki hiyo.

“Uwepo wa miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza wafanyakazi  tuliokuwa nao toka mwanzo hadi leo, na kwa heshima ya pekee  Mama Victor na Mrs Mitemo  ndiyo watakao kata keki hii” alisema Mtei.

Keki hiyo ilikatwa na wafanyakazi   hao  Monica  Victor   na Pili Mitemo  ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu.

Aidha, kwa upande  Clouds FM, iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa nchini hasa kwa kuwasaidia wasaidia wasanii kufikia malengo yao.

Kwa upande wake  Ibrahim Tuwa ‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha  shughuli hiyo, aliwaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono na wataendelea na huduma bora zaidi ha hapo. Dj Ibra alijiunga na Bilicanas tokea 2002,ambapo mpaka sasa ana miaka 10 kwenye klabu hiyo  iliyowahi kuwa na madj maarufu waliopita  hapo ambao wengi wao wapo kwenye vituo vya televisheni na redio.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.