Habari za Punde

*TASWA FC YAKUBALI KICHAPO CHA MABAO 4-0 KUTOKA KWA MAVETERAN WA BAGAMOYO


Kikosi cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za Mizhezo TASWA FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki kati yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jana jioni. Katika mchezo huo TASWA FC imekubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa maveterani hao  wa mjini Bagamoyo, Timu ya Waandishi wa habari ya TASWA FC imeshiriki katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya mkutano wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika leo  kwenye hoteli ya Kiromo View mjini Bagamoyo ambapo utafunguliwa na Ridhiwani Kikwete na Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndugu Assah Mwambene.
Kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran.
Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba Ibrahim Masoud katikati akizungumza na Mzee Willy Chiwango kutoka gazeti la This Day (kushoto) ni Beny Kisaka mkurugenzi mwanadamizi gazeti la Jambo Leo.
Mkuu wa Wilala ya Bagamoyo Ahmed Kipozi (wa pili kulia) akizungumza na mwandishi mkongwe kutoka Zanzibar, Said Salim, huku wanahabari wengine wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mchezaji wa timu ya TASWA FC Juma Pinto, akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Bagamoyo Veterani katika mchezo huo uliofanyika kwenyeuwanja wa Mwanakerenge mjini Bagamoyo.
Mchezaji wa timu ya TASWA FC, Shafii Dauda (kushoto) akimiliki mpira huku beki wa timu ya Bagamoyo Veterani akiuwania katika mchezo huo, katikati ni mchezji wa timu ya TASWA FC Mohamed Akida.
Mshauri wa timu ya TASWA FC Masoud Sanani, akihimiza wachezaji wa TASWA FC kucheza kwa bidii baada ya kuchapwa magoli 4-0 huku wachezaji wa timu hiyo wakishangaa wasijue la kufanya wakati zikiwa zimesalia dakika za majeruhi

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.