Mkurugenzi
wa Prime Time, Joseph Kusaga akikabidhi hundi ya sh milioni 105 kwa makamu
mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga kwa ajili ya kutumika katika mkutano mkuu wa
klabu hiyo uliopangwa kufanyika Januari 19, mwakani.
************************
Kampuni
ya Prime Time Promotion imeikabidhi mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na
Kati, Yanga hundi ya shs Milioni 105 kwa ajili ya kutumika katika mkutano wake
mkuu wa mwaka wa wanachama uliopangwa kufanyika Januari 19,
mwakani.
Fedha
hizo zilikabidhiwa katika mkutano maalum uliowakutanisha viongozi wa Yanga na wa
kampuni hiyo uliofanyika kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo,
Jangwani.
Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kuwa klabu yake imeingia makubaliano
na Prime Time kwa kusimamia shughuli zake zote ikiwa pamoja na mkutano
huo.
Sanga
alisema kuwa mbali ya mkutano huo, Prime Time itakuwa na jukumu la
kuandaa mechi mbali mbali za kimataifa kwa ajili ya kuhimarisha kikosi chao na
baadhi ya malipo yatachukuliwa na kampuni hiyo.
Alisema
kuwa hatua hiyi ni ya kuifanya klabu yao kuwa ya kisasa zaidi na
kutambua kampuni zenye uwezo wa kufanya shughuli mbali mbali kama Prime Time
Promotion kufanya kwa niaba yao.
“Kuna
kampuni zenye uwezo au utaalam wa kufaya matukio mbali mbali kama Prime Time
ambazo zinatakiwa kupewa nafasi hiyo, uongozi hauwezi kufanya shughuli zote,
tunataka kuendesha klabu kisasa zaidi,” alisema Sanga.
Nae
Mkurugezi wa Prime Time Joseph Kusaga alisema kuwa makubaliano hayo yatahusisha
pia mechi ya kimataifa itakayofanyika Januari 12 na 13 na shughuli nyingine za
klabu hiyo ili kuongeza kipato.
Kusaga
alisema kuwa wamevutiwa na Yanga kutokana uongozi wao kuongoza kwa uwazi zaidi
na kuvutiwa hatua yao ya hivi karibuni ya kuweka mapato na matumizi wazi kwa
wanachama na wadau wa michezo kwa ujumla.
Alisema
kuwa huu ni mwanzo tu kwani kwa mwaka 2013 wamejipanga kufanya kazi na vilabu
vyote nchini ili kukuza na kuendeleza mchezo huo. Kituo cha Televisheni cha
Clouds kinatarajia kuonyesha live mkutano huo.
No comments:
Post a Comment