Hali ya Baridi imezidi katika Jiji la Istanbul, nchini Uturuki ambapo imeelezwa kuwa hadi jana usiku ilifikia nyuzi joto 3, na kuwafanya wakazi wa jiji hilo kushindwa kufanya shughuli zao kwa kutotoka nje. Katika picha hizi ni baadhi tu ya picha zilizopigwa eneo la Mitaa ya Basiktas Istanbul, jana usiku. Mtandao huu unapenda kuwaondoa hofu mashabiki, wapenzi na wote wa Timu ya Yanga, ambao wanahisihali hii itawasumbua wachezaji wa timu hiyo. Ni kwamba hali hii ya baridi kali ipo katika Jiji la Istanbul tu kama ilivyo kwa nchi yetu ya Tanzania, ambapo Jiji la Dar es Salaam, lina hali ya hewa tofauti na mikoa mingine, ambapo Timu ya Yanga ipo katika mji wa ANTALYA, na hadi sasa meelezwa kuwa bado barafu ipo na inazidi kadri muda unavyosogea.
Mji huo jinsi unavyoonekana ukiwa hauna watu kutokana na na baridi kuzidi kuwa kali.
Sehemu ya magari yakiwa yamejaa barafu...
Baadhi ya wakazi wa Istanbul, wakionekana mmoja kwa mmoja katika mitaa ya Basiktas.
Magari yakiwa yamejaa barafu....
Barafu ikiwa imetanda eneo la njia na maduka...
Hii ni hali halisi inayoendelea kwa sasa katika jiji la Istanbul......
Magari yakiwa na barafu.
No comments:
Post a Comment