Habari za Punde

*KINANA ASHIRIKI KAZI ZA KIJAMII KIBONDO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kumwambo, Wilayani Kibondo, Jana, baada ya kushiriki ujenzi wa chumba cha darasa, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Bunyambo Wilayani Kibondo, Jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Wengine ni baadhi ya viongozi na wananchi aliofuatana nao kwenye msafara wake. 
 Baadhi ya wazee, watendaji na wajumbe wa mashina wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Maendeleo wa Kibondo, Jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma. 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na msafawa wake, wakinunua miwa njiani baada ya kukutana na muuzaji wa miwa hiyo, wakati wakitembea kwa mguu zaidi ya kilometa moja kwenda kwenye mkutano wa hadhara Kijiji cha Bunyambo, baada ya kushiriki shughuli za ujnezi wa Ofisi ya CCM katika kijiji hicho, Wilayani Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma. Picha na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.