Habari za Punde

*MATUKIO KATIKA PICHA YANGA ILIPODHIHIRISHA VITU VYA UTURUKI CCM KIRUMBA MWANZA LEO

 
Golikipa wa timu ya Black Leopards, Posnett Omony, akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete, kwa njia ya penati.Timu ya Yanga imeibuka kidedea kwa kuinyuka Black Leopards mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa leo jioni kwenye Uwaja wa CCM Kirumba. Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Said Bahanuzi.
 Wachezaji wa timu Yanga wakishangilia bao la pili lililofungwa na Jerry Tegete, katika  kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende (kulia) akipiga krosi huku Moses Kwena wa Black Leopards, akijaribu  kumdhibito wakatia wa mchezo huo uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani na kuandika bao la kwanza.
 Hamis Kiza wa Yanga (kushoto) akifanya jitihada za kumtoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
 David Luhende wa Yanga (kulia) akimdhibti, Moses Kwena, wa Black Leopards.
 Baadhi ya mashabiki wa Soka wakiwa katika foleni ya kununu tiketi na ili kuingia uwanjani kujionea kandanda safi kati ya timu ya Yanga na Black Leopards ya Afrika kusini.
 Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
Sehemu ya umati wa mashabiki 
 Mtanange ukikaribia kuanza.
 Kikosi cha timu ya Black Leopards.
 Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika ngua kuchanika,mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete akiwatoka mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry alifanikiwa kufunga goli la pili.

  Nginja nginja tuu
 Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kuisha.
 Sehemu ya Umati wa mashabiki wa timu ya Yanga.
 Mashabiki wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia uwanjani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.