Mjasiriamali Elizabeth Chami (26), akioka keki kwenye jiko la kisasa alilozawadiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012, kwenye karakana yake iliyopo Tabata Mawenzi, Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa karakana hiyo, Happiness akiandaa keki kwenye jiko hilo la kisasa.
Mfanyakazi wa Kiwanda cha kutangeneza Shampoo cha L &, V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam, Hashim Hussein, akipaki katoni za bidhaa hiyo. Kiwanda hicho kilisaidiwa chupa 15,000 baada ya mmiliki wa kiwanda hicho Valerian Luzangi (hayupo pichani) kuwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012.
Luzangi, akisaidia kupanga vizuri chupa zilizojazwa shampoo. Kushoto ni mfanyakazi wa kiwanda hicho Stahabu Mwinyi.
Mjasiriamali Valerian Luzangi (38), kulia, akipanga vizuri katoni za shampoo anazozalisha katika kiwanda chake cha L & V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Luzangi alisaidiwa chupa 15,000 baada ya kuwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012, Kushoto ni mfanyakazi wake, Hashim Hussein.
Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha, wakiweka sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba ya zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012.
Mjasiriamali Innocent Mberwa akionesha tikiti maji katika moja ya mashamba ya Kampuni yao ya Tin Wax yaliyopo eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo wa maji wa umwagiliaji baada ya kushinda promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Baadhi ya vitunguu vinavyozalishwa katika shamba hilo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO.
No comments:
Post a Comment