Wakazi wa Reading, nchini Uingereza wamejumuika kwa pamoja na kufurahia kwa kucheza michezo ya kuteleza katika barafu, iliyodondoka kwa wingi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Baada ya barafu hiyo kudondoka kwa wingi na kuleta tafrani nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya wakazi wa mji wa Reading badala ya kuendelea kulalamikia usumbufu uliotokana na kusitishwa kwa huduma muhimu kama usafiri wa anga, treni, barabara na shule kufungwa, maduka n.k, wananchi hao waliamua kujumuika kwa pamoja katika barafu hizo na kufurahia mchezo wa kuteleza katika barafu hizo (Bobsleighing).
Mchezo huu mara nyingi umekuwa ukifanyika katika nchi za baridi kali kama, Norway, Canada, Urusi na nyinginezo.
Sehemu ya barafu hiyo......
Sehemu ya wanafamilia waliojitokeza kufurahia mchezo wa kuteleza, hapa ni mama na mwanae wakiseleleka......
Mtoto akijiachia......
Hawa wakijiandaa kuanza kuteleza....
Michezo ikiendelea. Picha na Urban Pulse
No comments:
Post a Comment