Timu hiyo ya Yanga, ikiwa na msafara wa watu 37, wachezaji 27 na viongozi 10 iliwasili majira ya saa 2 asubuhi Ndege ya Shirika la ndge la Fast Jet ambapo leo jioni timu hiyo inatarajia kufanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Mchezo huo utakuwa ni wapili na wa mwisho wa kujipima nguvu kwa timu hiyo ya Yanga, kabla ya kuanza mchakamchaka wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, unaotarajia kuanza Jumamosi ya Januari 26, mwaka huu.
Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-2, huku mawili kati ya hayo yakiwekwa kimiani na Jerry Tegete, na moja likifungwa na Frank Domayo.
Black Leopard amabyo inajiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya PSL nchini Afrika Kusini iliomba kupata mchezo mwingine wa kirafiki ambapo kampuni ya Prime Time Promotions walioandaa ziara ya timu hiyo walikubaliana na Yanga mchezo huu ufanyike jijini Mwanza ili kutoa fursa kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuweza kupata burudani ya soka kutoka kwa timu hizi mbili.
Viiongillio vya mchezo huo vitakuwa ni Sh. 10,000/= kwa Jukwaa Kuu na Sh. 3,500/= kwa mzunguko.
No comments:
Post a Comment