Habari za Punde

*YANGA YAZIDI KUJIFUA UTURUKI YAWAVUTIA MAKOCHA WA NCHINI HUMO


Wachezaji wa Young Africans wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao kwenye ufukwe wa Fame Residencxe, leo asubuhi.
Kikosi cha Young Africans Sports Club, kimeendelea na mazoezi yake leo katika uwanja wa Fame Residece Football uliopo Antalya na kisha jioni timu ikaenda kufanya mazoezi katika ufukwe wa bahari, eneo lililopo nyuma ya hoteli ya Fame Residence, ikiwa ni siku ya tatu katika ziara ya mafunzo nchini Uturuki kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga mholanzi, Ernie Brandts, amesema anafurahishwa na maendeleo ya kambi, kwani toka wameanza mazoezi jumatatu wakiwa nchini Uturuki ameona mabadiliko makubwa kwa wachezaji wake, huku akisema hofu iliyokuwepo kwa watanzania juu ya hali ya hewa ya baridi kali si kweli kwani hali ya hewa katika mjii huo ni ya baridi kiasi tu na hata leo katika mazoezi ya asubuhi palikuwa na jua la kawaida.

Wachezaji wanaendelea kuzoea mazingira, na kujifunza mambo mengi yanayohusu soka kwani wageni mbalimbali waliofika katika mji huo wamekuwa wakipenda kujua mengi kuhusiana na timu ya Young Africans na soka la Tanzania kwa ujumla.
Wachezaji wakiwa mazoezini Ufukweni Majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki, timu ilifanya  mazoezi ya ufukweni katika ufukwle wa Hotelu ya Fame Residence  pemebezoni mwa Bahari ya Mediteranian.


Kocha wa makipa wa timu ya Bayern Leverkusen, Detier Gansi, jioni alishuhudia Young Africans ikifanya mazoezi ya ufukweni ambapo alisema amefurahia kuifahamu timu ya Yanga na wachezaji wake wanaonekana kuwa na morali ya kucheza soka, hivyo anaamini ziara hiyo itaisaidia timu kuwa pamoja na kujiandaa vyema na ligi alisema.
Wachezaji wakiwa katika mazoezi ya asubuhi uwanja wa Fame Residence Footbal.
























Wakati huo huo mchezaji wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima, amewasili jana jioni kwa ajili ya kuungana na wenzake kufuatia kuchelewa kuunganisha ndege siku ya jumamosi usiku akitokea nchini Rwanda alipokuwa amekwenda kuichezea timu yake ya Taifa.

Habari na Picha kwa hisani ya www.youngafricans.com

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.