Na
Mroki Mroki, FK BLG Kigoma
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula amewasili
mkoani Kigoma asubuhi hii kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na
kupongeza mabadiliko makubwa yaliyopo mkoani humo hasa Uwanja huo wa Ndege
ambao unaonekana sasa kuwa wa kisasa.
Mangula
ambaye amepata mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nappe Nnauye pamoja na mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho ambaye ni
Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma, Kanali Mstaafu. Issa Machibya pamoja na viongozi mbalimbali wa chama
na serikali.
Mangula
amesema Kigoma ya sasa si Kigoma aliyo ijua miaka iliyopita na viongozi
wanastahili pongezi kwa maendeleo hayo ya sekta mbalimbali.
“Kigoma
ya leo sio Kigoma ile ya zamani ..uwanja huu wakati ndege inataka kutua
nilitaraji nitasikia matairi ya kihangaika lakini nikashangaa tunakwenda vizuri
tu” alisema Mangula akishangiliwa na wakazi wa Kigoma.
Aidha
amewaambia wakazi wa Mkoa wa Kigoma kutembea kifua mbele kutoka na mafanikio
makubwa yaliyofikiwa hasa katika ujenzi wa uwanja wa ndenge wa kigoma ambao
zamani haukuwa na tabaka la lami ambapo sasa uwanja huo umewekewa tabaka la
lami na kuondoa usumbufu waliokuwa wakiupata zamani wananchi wa Kigoma.
Pia
Mangula amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kupuuza kejeli zinazoendelea
kutolewa na wanasiasa wa upinzani kuwa mkoa wa kigoma umesahaurika kitu ambacho
amesema hakina ukweli kwani mkoa huo sasa umefunguka kwa miundombinu ya
barabara.
Wakati
huo huo, katika kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ccm,
mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili kesho mkoani hapa kwa
ajili ya maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Jumapili Februari 3, 2013
katika uwanja wa Michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea ambapo sasa yamefikia asilimia zaidi ya
themnini na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pamoja na wajumbe wa NEC
na viongozi wengine wa CCM wanataraji kwenda kukagua maandalizi hayo jioni ya
leo.
Mangula akiteremka katika ndege.
Akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Mangula akisalimiana na Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula akisalimiana
na viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege Mjini Kigoma
hii leo.
Makamu
Mwenyekiti wa UWT, Dogo Mabruk (kushoto) na Mjumbe wa NEC-Wilaya ya
Uvinza, Asha Baraka pamoja na wanachama wengine wa CCM wakimsikiliza
Mangula.
Vijana wa CCM waliofika kumpokea Makamu Mwenyekiti CCM Bara.
No comments:
Post a Comment