Habari za Punde

*MALINZI AZUNGUMZA NA WANAHABARI KUHUSU KUENGULIWA KWAKE KUWANIA URAIS WA TFF


 Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na baadaye kuenguliwa kugombea nafasi hiyo na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi huo, Jamali Malinzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo asubuhi kuhusiana na uamuzi huo na kusema kuwa maamuzi hayo ameyasikia tu kwa vyombo vya Habari lakini hadi sasa hajapata barua rasmi ya kuenguliwa kwake kuwania nafasi hiyo. 

Vile vile madai yaliyotolewa hadi kuenguliwa kwake sio  sahihi kwani sifa zote anazo. Malinzi ni mmoja kati ya waliokuwa wagombea nafasi ya Urasi wa TFF walioenguliwa na Kamati ya Uchaguzi , jambo ambalo jana lilizua mtafaruku kwa baina wa mashabiki wa Soka wa timu za Yanga na Simba walioungana kumtetea Malinzi kurejeshwa katika mchakato wa kuwania nafasi hiyo, huku mashabiki hao wakitoa kauli kuwa asiporejeshwa basi damu itamwagika.
Malinzi akiendelea kumwaga sera zake kuhusu kuenguliwa kwake.
Wanahabari wakinasa sauti ya Malinzi kupitia spika zilizopo ukumbini hapo leo asubuhi.
Wote walikuwapo.......
Waandishi wa habari za michezo kutoka vyombo mbalimbali wakiwa bize kukoti kila kinachozungumzwa na Malinzi, wakati wa mkutano huo.
Usikilizaji kwa umakini mkubwa.
Kutafakari kwa umakini...
Picha zote na Father Kidevu Blog.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.