Habari za Punde

*YANGA YAVUTWA SHATI NA MTIBWA SUGAR YATOKA SARE YA 1-1

KUKOSA mabao ya wazi kipindi cha kwanza kumeigharimu timu ya Yanga, iliyolazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa sare hiyo sasa Yanga imepunguza kasi yake iliyoanza nayo katika mchezo wake wa kwanza wa mzunguko wa pili, ilipoibanjua Tanzania Prisons, mabao 3-1.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa,Mtibwa ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao lake katika dakika ya 44 kupitia kwa Shaban Kisiga, aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Issa Rashid.
Kipindi cha kwanza cha mchezo huo, timu zote zilifanya mashambulizi ya kupokezana, huku Yanga ikipoteza nafasi za wazi kupitika kwa wachezaji wake Didier Kavumbagu, Jerry Tegete na Simon Msuva, na Mtibwa nao wakipoteza kupitia kwa Kisiga, Rashid Gumbo, Vicent Barnabas na Hussin Javu.
Hata hivyo, timu hizo zilikwenda mapumziko kwa Mtibwa kuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa kasi zaidi huku Yanga ikionekana kuwa na uchu wa kutaka kufunga mabao lakini safu ya ushambuliaji ilishindwa kutikisa nyavu za Mtibwa Sugar.
Hamis Kiiza aliisawazishia Yanga bao katika dakika ya 84, huku Yanga ikiutawala zaidi mchezo huo.
Kwa matokeo hayo Yanga inaendelea kuongoza ligi hiyo ikiwa na jumla ya pointi 33 ikifuatiwa na Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 30.
Kikosi cha Yanga:Ali Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Athuman Iddy ‘Chuji’, Frank Domayo, Simon Msuva, Didie Kavumbagu, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.
Kikosi cha Mtibwa:Hussin Sharif, Said Mkopi, Issa Rashid, Rajab Mohammed, Salum sued, Shabn Nditi, Vicent Barnabas,Rashid Gumbo, Hussein Javu, Shaban Kisiga na Ally M ohammed

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.