Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo
Seehemu ya wageni waalikwa na wanafunzi na wafanyakazi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo.
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Mama Koku Kairuki akimkabidhi tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo.
No comments:
Post a Comment