Habari za Punde

*JAPHET KASEBA KUPANDA ULINGONI MWEZI JUNI KUZIPIGA NA JOSEPH MAGUDHA WA KENYA


Boia wa kike, Peo Njau, ambaye ni msaidizi wa Mwandaaji wa pambano la ngumi kati ya Japhet Kaseba na Kamanda, akiwasainisha mikataba baadhi ya mabindia watakaocheza michezo ya utangulizi katika pambano hilo, wakati wa zoezi hilo lililofanyika leo mchana kwenye Kambi ya Kaseba Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Bondia Kamanda wa Makanda (kushoto) akitunishiana misuli na Ibrahim Maokola, baada ya kusaini pambano lao.
Bondia Japhet Kaseba, anatarajia kupanda ulingoni kwa mara nyingine mwanzoni mwa mwezi wa sita kuzipiga na bondia kutoka kenya,  Joseph Magudha, katika pambano la kimataifa la Raundi 12. 

Akizungumza na mtandano huu kuhusu maandalizi ya pambano hilo, mwandaaji msaidi Pendo Njau, alisema kuwa hivi sasa wamekwishaanza maandalizi ya mchezo huo wa kimataifa na tayari Bondia Joseph, kutoka nchini Kenya amekwisha thibitisha kutua nchini kukabiliana na Kaseba.

Aidha, Njau, alisema kuwa hivi sasa wameanza kuwaandaa mabondia wa nyumbani watakaocheza mechi za utangulizi ikiwa ni pamoja na kuwafua kwa mazoezi ya kutosha ili waweze kuonyesha mchezo mzuri siku hiyo.

''Katika mchezo huo,  mwanzoni maokola alikuwa amepangwa azipige na bondia kutoka mkoani morogoro na kamanda kupewa bondia mwingine, lakini kulitokea kupishana kwa maneno kati ya mabondia hao kiasi cha kutaka kupigana kavu wao kwa wao, jambo lililofanya sisi waandaaji kuona kuwa kuna umuhimu wa kuwaandalia pambano ili waweze kumaliza ubishi wao'' . alisema Njau

Aliyataja mapambano yaliyokwisha kamilika kuwa mpaka sasa mapambano ya utangulizi inategemea kuwa juma seleman atakayezipiga na Issa Omar,Juma Fundi atapigana na Moro Best, Yohana Mathayo, atazipiga Joseph Onyango kutoka Kenya. 
Na mapambano mengine yatajulishwa hapo baadae zoezi la usainishaji mikataba likikamilika

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.