*Western union yakabidhi zawadi kwa wshindi wa promosheni ya UEFA
Mkuu wa Huduma za Usafirishaji Fedha wa Benki ya DTB, Chandni Jiwa (wa pili kushoto) akikabidhi tiketi ya kwenda na kurudi Uholanzi kwa Quraish Omari Shindo mmoja wa washindi wa promosheni ya Shinda Tiketi Kuona Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) iliyokuwa ikiendeshwa na Western Union katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Masoko na Utafiti wa Benki ya Watu wa Zanzibar (TBZ), Seif Suleiman Mohammed na Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Samora), Deo Kayega.
******************
Na Mwandishi
Wetu
WESTERN Union leo imekabidhi zawadi ya tiketi kwa wateja wake wawili waliojishindia tiketi hizo kwa ajili ya kwenda kushuhudia fainali za kombe la UEFA, zinazotarajia kufanyika nchini Uholanzi
katika Uwanja wa Amsterdam.
Washindi hao waliokabidhiwa tiketi zao leo hii ni pamoja na Malik Gumbo na Ptropa Ndashau ambao wamejishindia tiketi hizo baada ya kuchezeshwa ka droo walishinda katika droo iliyofanyika leo mchana jijini Dar es Salaam, huku washindi wengine kumi wakijishindia ving’amuzi vya Star
Times.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa droo hiyo, msemaji wa Western Union, Monte Bilal, alisema kuwa, ndiyo kwanza wameanza Promosheni ya kampeni hiyo kubwa hapa nchini.
“Tunawapongeza
washindi na tunawatakia kila la kheri katika maandalizi ya safari yao kuelekea Amsterdam,”
alisema.
Aidha alieleza kuwa Western Union itagharamia mahitaji yote ya washindi hao, katika safari ya
kwenda kuangalia fainali hiyo.
Pia alisema kuwa washindi waliojishindia ving’amuzi, wao watapata nafasi ya kuangalia fainali
hizo kupitia luninga zao majumbani.
Aliwataja washindi hao kuwa ni Masuma Remtulla, Nicetus Joseph, Mary Kibona, Khalfani Kayoka, Priti Parekh,
Abilahi Salum, Sakina Abod, Tabu Tambwe, Zulfa Semboja na Scholastica Mbuga.
Msemaji wa Western Union, Monte Bilal, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo ya kutangaza washindi waliojishindia tiketi hizo.
No comments:
Post a Comment