Habari za Punde

*BUYERN MUNICH MABINGWA WAICHAPA BORUSSIA DORTMUND 2-1

 Mshambuliaji wa Timu ya Buyern Munich, Arjen Robben, (katikati)  Thomas Mueller (kushoto) na  Franck Ribery, wakishangilia kwa pamoja bao la Robben, alilifunga kipindi cha pili wakati wa mchezo wa Fainali wa Ligi ya Mabingwa kati yao na Borussia Dortmund, uliochezwa usiku huu kwenye Uwanja wa Wembley. Katika mchezo huo Buyern wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutwaa Kombe hilo.
Kipa wa Bayern, Manuel Neuer, akizuia shuti la mchezaji wa Dortmund, Robert Lewandowski (kushoto)  
 Mchezaji wa Bayern, Bastian Schweinsteiger, Kulia) akiruka na mpira wakati wa mchezo wa Fainali wa Ligi ya Mbingwa kati ya Borussia Dortmund na Bayern Munich uliochezwa kwenye Uwanja wa  Wembley London, usiku huu. Katika mchezo huo Bayern wameibuka na ushindi wa mabao 2-1, na kutwaa Kombe hilo.
Mshambuliaji wa Buyern Munich, Mario Mandzukic, (kulia) akifunga bao.
 Arjen Robben akidhibitiwa na wachezaji wa Borussia Dortmund's Neven Subotic na Lukasz Piszczek (kulia)
 Arjen Robben (kushoto) na Mario Mandzukic, wakishangilia.....
 Mchezaji wa Buyern Munich, Franck Ribery (kulia) akiruka kwanja................
Arjen Robben (katikati) akimchambua Kipa wa Dortmund, Roman Weidenfeller na kufunga bao la pili, wakati wa Fainali hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.