Bondia Francis Cheka, akimpeleka chini mpinzani wake Thomas Mashali katika raundi ya saba na kunusurika kutoka nje ya ulingo, wakati wa pambano lao la kuwania ubingwa wa IBF lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam. Katika pambano hilo Cheka alishinda kwa KO katika raundi ya 10 kati ya 12.
Bondia Thomas Mashali, naye akijibu mashambulizi mara tu baada ya kurudi ulingoni aliponusurika kutoka nje ya Ulingo, ambapo katika raundi hii aliweza kuonyesha uhai na kufufua matumaini kwa mashabiki wake kuwa angeweza kumaliza pambano hilo.
Shabiki namba moja wa Francis Cheka kutoka Mkoani Morogoro, akitoa sauti kumuelekeza bondia wake Cheka kufanya anavyohisi yeye.
Katika pambano hili pia palikuwa na vituko kibao na ubabe wa aina yake, Hapa askari Polisi na raia wakimburuza mpiga picha za video wa Kituo cha Televisheni cha Chanel 5, ili ashuke kutoka katika kona hii kwa madai 'eti' anawaziba watazamaji, huku askari huyu wa (kushoto chini) akipiga ngumi, ''Naona alijihisi kuwa na yeye ni Cheka na akasahau kuwa yeye ni mlinda usalama na amani mahala hapa''.
Askari hawa na raia baada ya kuona mpiga picha huyu amezidi kuwa mtata na kuwazidi nguvu, huku pambano hilo likisimama kwa muda, waliamua wote kwa pamoja kushika koti lake na kuanza kumvuta ili aanguke chini.
Hapa masumbwi yakiendelea baada ya Mpigapicha huyo kuamua mweeeenyewe kushuka eneo hilo, baada ya jamaa wote kushindwa kumshusha kama walivyotaka kufanya.
Palikuwa hapatoshi ulingoni hapa kwani kila Bondia alikuwa akishambulia kwa zamu na kila aliyeachia konde lilisikika kwa mashabiki kwa uzito uliokuwa ukitoka mkononi mwa bondia.
Ebwa eeeeh!!! kaiona hiyo.........
Konde zito lililoachiwa na Cheka liliweza kumpeleka chini kwa mara nyingine mpinzani wake Mashali, katika raundi ya Nne.......
Kuna wakati Bondia mmoja alikuwa akimwonea mwenzake kwa sekunde kadhaa mfululizo kama hapa, ilikuwa ni zamu ya Cheka kushambulia mfululizo.
Ebwana eeh! Mashali alishindwa kuvumilia na kupelekwa chini na hapa, alikuwa akihesabiwa na mwamuzi, ambapo alimudu kuamka na kuendelea na pambano........
Lakini katika raundi ya kumi, Mashali alipelekwa chini kwa mara nyingine na hapa sasa ndiyo ilikuwa wa pambano hilo kwani jamaa, alishindwa kabisaaa kuinuka huku akionekana kana kwamba amepoteza fahamu na mwamuzi kuchukua maamuzi ya kumvua kifaa cha kulinda meno na kuonyesha ishala ya kumaliza pambano hilo. Ndipo shangwe na nderemo kutoka kila kona ya ukumbi huo ziliripuka huku mashabiki wengine nao wakianza kutimua mbio kuwahi kutoka ndani ya ukumbi huo kwa kuhofia usalama wao na vurugu, kutokana na ukumbu huo kuvunja rekodi ya mapambano yote yaliyowahi kuchezwa katika ukumbi huo kwa kufurika watu.
Hili lilikuwa ni moja kati ya mapambano ya utangulizi kati ya Amos Mwamakula kutoka Kinondoni (kulia) na Ibrahim Class wa Ilala. Hapa Amos akiachia 'Apakati', kwa mpinzani wake, lakini katika pambano hili, Ibrahim Class (kushoto) aliibuka na ushindi kwa pointi.
Pambano la utangulizi ambalo pia lilikuwa ni la raundi nane na la upinzani na kuvutia.....Amos na Class.
Amos na Class, wakiendelea kushambuliana....
Hili pia lilikuwa ni pambano lenye upinzani mkubwa kutokana na mabandia hawa kuwa ni wadogo wa mabondi wa 'Main Ring' (kushoto) ni Charles Mashali akipambana na Cosmas Cheka, katika pambano la raundi 6. Katika pambano hilo Cosmas, alishinda kwa pointi na kumsafishia njia ya ushindi Kaka yake, Francis Cheka.

Shabiki wa Kina Cheka, akimhamasisha Cosmas cheka kumshambulia atakavyo mpinza wake Charles Mashali.
Cosmas Cheka, akiruka kushangia ushindi baada ya kutangazwa kumbwaga mpinzani wake kwa pointi.
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia pambano hilo, ambao hawakuweza kufaidi kulingana na pesa ya kiingilio waliyolipa ya VIP huku huduma ikiwa ni kiingilio cha kawaida, kwani wengine walilazimika kununua viti na wengine kukaa chini.
Msanii wa Filam (kushoto) akiwa amekaa chini wakati alilipa kiingilio cha VIP sh. 10,0000, baada ya kukosa kiti huku eneo hilo likiwa limejaa kupita kiasi.
Sehemu ya mashabiki wa masumbwi waliojitokeza kushuhudia ndonga hizo......
Msanii wa Hip Hop Profesa Jay, akiwa ni mmoja kati ya mashabiki waliokuwapo ukumbini hapo kushuhudia ndonga hizo jana usiku.
TID naye alikuwapo, hapa akiwa amesimama baada ya kukosa siti.......
Msanii wa Hip Hop Inspekta Harun, akiwa ni mmoja kati ya mashabiki waliokuwapo ukumbini hapo kushuhudia ndonga hizo jana usiku.
Warembo pia walikuwapo kushuhudia ndonga hizo.........
Hili lilikuwa ni moja kati ya pambano la utangulizi.........
Japo wengine walikuwa na tiketi zao mkononi, lakini bado walishindwa kuingia ukumbini humo na kulazimika kushuhudia ndonga hizo nje ya geti kubwa........
Huu ni usafiri wa pikipiki za mashabiki waliozama ndani kushuhudia ndonga hizo......



























No comments:
Post a Comment