Habari za Punde

*SPORTS EXTRA NA SPORTS BAR MEI MOSI BONANZA YAFANA VIWANJA VYA LEADERS CLUB KINONDONI


 Leo timu mbalimbali za jijini Dar zimekutana na kumenyana katika Bonanza la Sports Extra na Sports Bar, katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni. Bonanza hilo limedhaminiwa  na Benki ya NMB, Kampuni ya simu za Mkononi, Vodacom, Bia ya Castle, Clouds Redio na Clouds Tv. 
 Kipa wa timu ya Tanesco, akipiga shuti kuokoa moja ya hatari langoni kwake.

 Kipa wa TBL, akiokoa hatari langoni kwake.
 Wachezaji wa Vodacom, wakipasha kujiandaa na mtanange wao......
 Kikosi cha Clouds Fm, kilichoshuka dimbani kuwakabili Simbanet.
 Kikosi cha Simbaneti, kilichokipiga na Clouds Fm.
 Mbwiga Mbwiguke (kulia) akipozi kwa picha na Shafii Dauda kabla ya kuanza mtanange huo.
 Shafii Dauda (kulia) akijikunja kuachia shuti mbele ya Beki wa SImbaneti, hata hivyo shuti hilo halikuzaa matunda.
 Luambano wa Clouds Fm, (katikati) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Simbaneti.
 Kipa wa Simbaneti, akiokoa mchomo.....
 ''We Babu hebu tulia kwanza''........
 Luambano (kushoto) akifunga bao.......
 Kipa wa Vodacom, akipanga ukuta wa mabeki wake wakati wa faulo iliyosababishwa na yeye mwenyewe baada ya kuudaka mpira aliorudishiwa akiwa ndani ya eneo lake na kupigwa kadi ya njano na kufungwa bao kwa njia ya adhabu ndogo.
 Salum Mwalimu, akiendelea kuimarisha ukuta wake.....
 Tangazo la wadhamini wa Bonanza hilo......
Salum Mwalimu, akifungwa bao.......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.